Mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amedai kwamba Cindy Sanyu hapaswi kupigiwa kura kama rais wa muungano wa wanamuziki nchini humo kutokana na mienendo yake isiyoridhisha.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Bebe Cool amesema Cindy ameshindwa kuwaunganisha wasanii nchini uganda lakini pia hapendi kukosolewa kwenye utendakazi wake.
Bosi huyo wa Gagamel amedai kwamba cindy ni kiongozi dikteta kitu ambacho amesema sio kizuri kwa kiongozi kuwa nayo.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Gyenvudde” amesema Cindy anapotofauti na mtu kimawazo, mtu huyo anakuwa adui wake, hivyo hapaswi kupewa nafasi nyingine ya kuwaongoza wasaniii wa uganda kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni.
Hata hivyo ameonekana kumchagua Cindy kuwa rais wa muungano wa wasanii nchini uganda badala ya king saha ambaye kwa mujibu wake ni mvuta bangi.
Utakambuka kwenye kinyanganyiro cha kuwania wadhfa wa urais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda wasanii watatu peke ndio wametia nia ya kugombea wadhfa huo kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni.
Wasanii hao ni pamoja na Daddy Andre, King Saha na Cindy Sanyu ambaye ndiye rais wa sasa wa muungano wa wasanii nchini Uganda.