Msanii mkongwe kwenye muziki Bebe Cool ameitaka serikali ya Uganda kufungua matamasha ya muziki mwezi Disemba mwaka huu.
Bebe cool amesema hatua hiyo itawasaidia wasanii kupata riziki ya kuwasaidia maishani ikizingatiwa kuwa mwezi huo ndio watu wengi huandaa sherehe nyingi.
Kauli ya Bebe Cool imekuja mara baada ya rais yoweri museveni kutangaza kwamba serikali yake inalenga kulegeza kanunu za kudhibiti msambao wa corona kwenye maeneo ya burudani na tasnia ya muziki kwa ujumla mwezi Januari mwaka wa 2021.
Ikumbukwe wasanii nchini Uganda hawajafanya matamasha ya muziki tangu mwezi Machi mwaka wa 2019 wakati serikali ilipiga marufuku matamasha ya muziki kama njia ya kudhibiti msambao wa corona.