You are currently viewing BEBE COOL ATHIBITISHA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA NA BABY MAMA WAKE ZUENA KARIMI

BEBE COOL ATHIBITISHA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA NA BABY MAMA WAKE ZUENA KARIMI

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amekuwa akiahidi kufanya harusi na mke wake Zuena Karimi kwa muda, na namna mambo yanavyoenda ni kama tutashuhudia harusi kubwa kati ya mastaa hao mwaka huu.

Kwenye moja ya onesho lake huko Mukono nchini Uganda Bebe Cool amethibitisha kuwa ndani ya mwaka huu ana mpango wa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi Zuena Karimi.

Bosi huyo wa Gagamel amewaambia mashabiki zake kuwa harusi ambayo anaenda kuifanya mwaka huu itavunja historia nchini Uganda.

Ni hatua ambayo imepokelewa kwa ukubwa na wafuasi wake wengi kwenye mitandao ya kijamii wakisema kwamba wanangoja harusi hiyo kwa hamu harusi ya wawili hao.

Utakumbuka Bebe Cool ni msanii pekee ambaye hajafanya harusi ya kanisani kando na mahasimu wake wa jadi Jose Chameleone na Bobi Wine.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke