You are currently viewing BEBE COOL ATIA NENO JUU YA SHEEBAH KUDHALALISHWA KINGONO

BEBE COOL ATIA NENO JUU YA SHEEBAH KUDHALALISHWA KINGONO

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amemshauri msanii mwenzake Sheebah kumburuza mahakamani mwanaume aliyemnyanyasa kingono kwenye moja ya performance yake wikiendi iliyopita.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Bebe Cool amesema mwanaume aliyemdhalilasha sheebah kijinsia alivuka mipaka, hivyo anapaswa kufunguliwa mashtaka ili iwe funzo kwa wanaowanyanyasa wanawake katika jamii.

Hata hivyo, amekataa kumuunga mkono Sheebah kwa madai aliyoyaiibua kwa kuwa shutuma za unyanyasaji wa kijinsia zinaweza tu kuthibitishwa na ushahidi uliowasilishwa kwa mamlaka husika.

Kauli ya Bebe Cool imekuja mara baada ya Sheebah Karungi kusimulia kisa kilichowagusa wengi kwa kusema kuwa alinyanyaswa kingono na mtu anayeheshimika katika jamii.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nkwata Bulungi (Bailamos)” alikuwa amepangiwa kutumbuiza kwenye sherehe ya mtu huyo ambaye jina lake halikutajwa lakini kabla hajapanda jukwaani, jamaa huyo alifika kwenye gari lake na kuanza kumpapasa bila ridhaa yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke