You are currently viewing BEBE COOL ATOA SOMO KWA WASANII WA UGANDA

BEBE COOL ATOA SOMO KWA WASANII WA UGANDA

Bosi wa lebo ya muziki ya Gagamel msanii Bebe Cool amewashauri wanamuziki wa Uganda kuhakikisha wanakubalika nchini kwao kwanza kabla ya kuupeleka muziki wao kimataifa.

Katika mahojiano na Urban TV, Bebe Cool amesema wasanii wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kuteka nyonyo za Waganda kabla ya kuanza kufanya muziki unaolenga soko la kimataifa.

Hitmaker huyo wa “Wire Wire” anaamini kuwa jambo hilo limemsaidia yeye, Bobi wine, pamoja na Chameleone, kupata pesa nyingi kupitia matamasha ya muziki ya ndani ya nchi.

Ikumbukwe Bebe Cool anatajwa kuwa miongoni mwa wanamuziki matajiri zaidi Afrika Mashariki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke