You are currently viewing BEBE COOL AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BIFU YA KING SAHA NA ALLAN HENDRICK.

BEBE COOL AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BIFU YA KING SAHA NA ALLAN HENDRICK.

Bebe Cool amekuwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka 20 bila kupoa.

Ni moja kati ya wasanii wakongwe ambao wakiongea chochote kila mtu kwenye tasnia muziki nchini Uganda anamsikiliza licha ya maisha yake kuandamwa na kashfa nyingi.

Msaniii huyo ametoa wito kwa kijana yake Allan Hendrik na King Saha wajitenge na vita vya maneno na badala yake wafanya muziki mzuri

Hitmaker huyo wa Gyenvudde amesema wawili hao wanapaswa kuelekeza nguvu zao zote kwenye muziki kwani kutupia maneno makali mtandaoni kutawapoteza kimuziki huku akitoa angalizo kwa King Saha aache kutumia dawa za kulevya.

“They have time to be productive because they are still young. They should focus on releasing music, they shouldn’t go after one another. I just want to  King Saha stay away from drugs,” Amesema kwenye mahojiano yake hivi karibuni.

Mapema wiki hii , Allan Hendrick alithibitisha kuwa hana ugomvi wowote na King Saha licha ya wimbo wake uitwao  ‘matayo’ kuonekana kumlenga moja kwa moja msanii huyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke