You are currently viewing BEBE COOL AWAJIBU WALIMWENGU KUHUSU ISHU YA KUTOMSAPOTI ALLAN HENDRICK

BEBE COOL AWAJIBU WALIMWENGU KUHUSU ISHU YA KUTOMSAPOTI ALLAN HENDRICK

Staa wa muziki nchini Uganda Bebe Cool amefunguka kuhusu ishu ya kutomsaidia mwanae Allan Hendrick kutunaua wigo wa muziki wake licha ya kuwa na ushawishi mkubwa Afrika Mashariki.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Bebe Cool amekanusha madai ya kumtelekeza Allan Hendrick kwenye muziki wake huku akisema amekuwa na ukaribu na mwanae huyo kwa muda akimpa ushauri wa namna ya kuboresha muziki wake na kubaki kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu bila kuchuja.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Gyenvudde” amesisitiza kuwa anaweza kuinua muziki wa Allan Hendrick bila hata kumpa kollabo tofauti na namna watu wamekuwa wakimshinikiza kwenye mitandao ya kijamii.

Kauli ya Bebe Cool imekuja siku cha baada ya Chameleone kumwagia sifa Hendrick kwa kipaji chake cha muziki ambapo alienda mbali zaidi na kuahidi kufufua muziki wake ambao umekuwa ukisuasua katika siku za hivi karibuni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke