Msanii mkongwe kwenye nchini Uganda Bebe Cool ni moja kati ya wasanii ambao wamekuwa kwenye tasnia ya muziki nchini humo kwa muda mrefu.
Bosi huyo wa Gagamel amekuwa na muendelezo mzuri wa kuachia kazi ambayo imemfanya kuwa gemu kwa miongo mitatu bila kuchuja.
Sasa akiwa kwenye moja ya Interview Bebe Cool amewshauri wasanii wachanga kuepuka kutegemea kolabo kama kweli wanataka kudumu kwenye muziki kwa muda mrefu.
Kulingana na hitmaker huyo wa Gyenvudde mashabiki wa muziki husahau haraka kolabo ikilinganishwa na nyimbo ambazo wasanii wanatoa kama wasanii wa kujitegemea.
Ikumbukwe Bebe Cool ana zaidi ya nyimbo 400 ikiwemo Kolabo.