You are currently viewing BEBE COOL AWASUTA VIKALI MAPROMOTA NCHINI UGANDA, ATISHIA KUSUSIA SHOWS ZAO

BEBE COOL AWASUTA VIKALI MAPROMOTA NCHINI UGANDA, ATISHIA KUSUSIA SHOWS ZAO

Mwanamuziki kutoka Uganda Bebe Cool amefunguka na kudai kwamba hatokubali kufanya shows anazolipwa kati ya shillingi laki moja na tatu za Kenya.

Hii ni baada ya mapromota wa muziki nchini uganda kuanza kuwalipa wasanii wa nigeria shillingi laki 4 za Kenya kwenye matamasha yao ya muziki.

Bebe Cool ameonyesha kusikitishwa na mapromota wa muziki nchini humo wanaoendelea kuwapa kipau mbele wasanii wa Nigeria kwenye matamasha ya muziki.

Akizungumza kwenye moja ya perfomance yake, Bebe Cool amewataja mapromota hao kama wanafiki, wasiowatakia wasanii wa Uganda mema.

Hitmaker huyo ngoma ya “Gyenvude” ameenda mbali zaidi na kuema kwamba kasumba hiyo huenda ikasambaratisha tasnia ya muziki nchini Uganda.

Bebe cool amewataka mapromota wa Nigeria kurudisha fadhila kwa wasanii wa uganda kwa kuanza kuwazingatia kwenye shoo zao kwa faida ya tasnia ya muziki ya nchini hizo mbili.

“Msanii wa Uganda anapoachia ngoma kali, mapromota huanza kuua brand lakini huwa wanawafuata sana wasanii wa Nigeria. Lakini mapromota wa Nigeria wanapaswa kurudisha fadhila kwa kucheza muziki wetu,” alisema.

Bebe Cool aliendelea kwa kusema “Tulijitahidi sana kujenga hii tasnia. Sasa imekua na watu wanatuangalia. Mapromota wanapaswa kututhamini na kuturuhusu kufurahia matunda ya bidii yetu,”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke