Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Bebe Cool alitangaza mwishoni mwaka 2021 aliahidi kuzindua tuzo yake ya kila mwaka kwa ajili ya kutambua juhudi za wasanii wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.
Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni Bebe Cool amesema ametanga shillingi millioni 127 za Kenya ambayo itatumika kuendesha shughuli ya kuzindua tuzo yake ambayo inatarajiwa kuanza mwaka huu.
Hitmaker huyo “Gyenvudde” amesema waasanii watatunukiwa pesa taslimu badala ya tuzo za glassi ambazo wamekuwa wakipewa na waandaaji wa tuzo zenye thamani ya takriban shillingi elfu 63 za Kenya.
“Tuzo za Uganda hazina maana. Nazindua tuzo yangu ambayo itakuwa tofauti. Tuzo ya Bebe Cool itaghrarimu kati ya shillingi billioni 1.5 hadi billioni 2 pesa za Uganda..alisema kwenye mahojiano na runinga moja nchini Uganda.
Bebe cool amesisitiza kuwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo tuzo yake itakuwa yenye bora afrika mashariki na kati.