You are currently viewing BEKA FLAVOUR AACHIA RASMI TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

BEKA FLAVOUR AACHIA RASMI TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva Beka Flavour ameanika hadharani tracklist ya Album yake mpya inayokwenda kwa jina la First Born.

Kupitia Instagram yake msanii huyo amechapisha Artwork ya Album hiyo ambayo ina jumla ya ngoma 15 ya moto huku ikiwa na kolabo 7 pekee.

Beka flavour amewashirikisha wakali kama Barnaba, Christian Bella, Naiboi, Linah, Young Lunya, na Yamoto Band huku Album yenyewe ikiwa na nyimbo kama Wivu, Medula, Dunia Tunapita na nyingine nyingi.

Hata hivyo hajataja tarehe rasmi ya kuiachia album hiyo zaidi ya kuwataka mashabiki kuendelea kusalia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi.

First Born ni album ya kwanza kwa mtu mzima Beka flavour kuitoa tangu aanze safari yake ya muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke