Mwanamuziki wa Bongofleva, Beka Flavour amedai kuwa video mbili za nyimbo zake, Libebe na Sikinai zimefutwa katika chaneli yake ya YouTube.
Beka flavour amesema hata alipowasiliana na YouTube amejibiwa kuwa video hizo zimefutwa na mtu ambaye wanafanya naye kazi.
Hitmaker huyo wa “In Love” amewatoa hofu mashabiki zake kwa kusema kuwa timu yake inajaribu kila wawezalo kuhakikisha video za nyimbo zinarejea youtube ila hana uhakika kama zitarejeshwa kwenye mtandao huo.
“Kwa hiyo hatujajua ni nani ambaye amezifuta video hizo, tunaendelea kupambana ziweze kurudi japo sina uhakika kama zitarudi,” amesema Beka.
Utakumbuka Beka Flavour alikuwa miongoni mwa wasanii wanne waliokuwa wanaunda kundi la Yamoto Band, akiwemo Aslay, Mbosso na Enock Bella.