Mwanamuziki wa Bongofleva, Beka Flavour amedai haweza kujihushisha na timu yoyote katika muziki huo ili kunufaika na mashabiki wa timu fulani kwani yeye anatengenezea kazi nzuri ambazo anajua zinaweza kupendwa na wote.
Beka Flavour amesema anafanya muziki mzuri kwa ajili ya mashabiki wake ambao wapo naye kwa ajili ya ubora wa kazi zao na sio timu ambazo kamwe hawezi kujiunga nazo.
Kwa miaka ya hivi karibuni wasanii Alikiba na Diamond Platnumz wamekuwa ni washindani wakubwa ambao wametengeneza timu ambazo hadi baadhi ya wasanii wengine wamejiunga nazo.
Ikumbukwe Beka Flavour alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliokuzwa na kituo cha Mkubwa na Wanawe chake Mkubwa Fella, na chini ya kundi la Yamoto Band ambalo lilikuwa linaundwa na wasanii Aslay, Enock Bellla na Mbosso ambaye alichukuliwa na lebo ya WCB Wasafi yake Diamond.