Mwimbaji wa Bongofleva, Ben Pol amejitokeza na kusema kuwa hajapata taarifa yoyote kuhusu kukamilika kwa talaka na aliyekuwa mke wake, Anerlisa.
Wiki iliyopita Anerlisa ambaye ni binti wa seneta wa Nakuru Tabitha Karanja alitangaza kuwa mchakato wa talaka yake na Ben Pol umekamilika.
“Mimi pia naona ripoti hizi mtandaoni. Sijafahamishwa rasmi au kwa njia isiyo rasmi. Sijui hayo mawasiliano aliyapata wapi maana hata mahakama niliyofungua kesi ya talaka haifahamu taarifa hizo,” Ben Pol aliambia Nation.
Utakumbuka wawili hao walifunga ndoa Mei 2020 katika Kanisa Katoliki la St Gaspar huko Mbezi Beach, Tanzania.