You are currently viewing BENDI YA WENGE BCBG YATANGAZA RASMI KURUDI KWENYE ULIMWENGU WA MUZIKI

BENDI YA WENGE BCBG YATANGAZA RASMI KURUDI KWENYE ULIMWENGU WA MUZIKI

Prodyuza wa muziki kutoka nchini Congo, Amadou Diaby ameanzisha harakati za kuifufua tena bendi kongwe ya muziki nchini humo Wenge BCBG.

Inaelezwa kuwa, Februari 28 mwaka huu, Amadou aliandaa kikako na wanachama wa bendi ya Wenge BCBG ambayo ilisambaratika miaka ya 90.

Kwa mujibu wa taarifa, Amadou ametia saini mkataba na wanabendi hiyo ambao walihudhuria mkutano wake ambao ulihudhuriwa na Adolph Dominguez, Ferre Gola na wengine. MChini ya mkataba huo, bendi hiyo itarekodi nyimbo kadhaa nchini Cape Verde na kuandaa matamasha katika sehemu mbalimbali za ulimwengu.

Tamasha la kwanza likitarajiwa kufanyika katika uwanja wa Stade Des Martyrs huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu, ambapo ni sikukuu ya kusherehekea Uhuru wa Taifa la kongo.

Kanda na hayo, mkataba huo pia unahusu kuandaliwa kwa filamu ya matukio halisi kuhusu bendi ya Wenge Musica tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 1979 hadi iliposambaratika na kukaanzishwa makundi mawili ambayo ni Wenge BCBG 4×4 na Wenge Maison Mère.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke