Msanii wa Sol Generation Bensoul amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ishu ya kumsaliti mpenzi wake Noni Gathoni baada ya kudaiwa kuwa alimpachika uja uzito mwanamke mmoja kaunti ya Mombasa.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nairobi” amekiri hadharani kuwa ni kweli kuna mwanamke ana uja uzito wake kaunti hiyo huku akisema kuwa ni makosa ambayo alifanya na mrembo mmoja aliyekutana nae kwenye performance yake huko Mombasa.
Bensoul ameenda mbali na kusema kwamba alikuwa na mpango kuweka wazi habari hiyo kwa umma ila mwanablogu mwenye utata nchini Edgar Obare alimpiku na kuchapisha taarifa hiyo kabla hajafanya hivyo.
Hata hivyo ameahidi kujitolea kusimamia suala nzima la kutoa matunzo kwa baby mama wake huyo hadi pale atakapojifungua.
Suala hilo limeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa hawaamini kama Bensoul anaweza jihusisha na udanganyifu kwenye mahusiano yake ikizingatiwa kuwa hajawahi patikana na skendo yeyote tangu aanze safari yake ya muziki.