Mrembo Tiffany Muikamba amethibitisha kuwa amejifungua mtoto wa kike.
Muikamba ambaye aliwahi kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Sol Generation Bensoul ameeleza furaha yake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kujifungua salama.
Ni hatua ambayo imepokelewa kwa furaha na mastaa wa muziki nchini pamoja na mashabiki ambao wamemtakia mrembo huyo pamoja na Bensoul salamu la pongezi kwa hatua hiyo kubwa maishani.
Utakumbuka taarifa za Tiffany Muikamba kuwa na uja uzito wa Bensoul zilibuka mwaka jana baada ya mrembo huyo kuanika wazi namna ambavyo walikutana na msanii huyo huko Mombasa, kitendo ambacho karibu ivunje uhusiano wa Bensoul na mpenzi wake wa siku nyingi Noni Gathoni.