You are currently viewing BENZEMA AFUNGUKA KUHUSU UTATA UNAOZINGIRA WIMBO WA FOTO MOTO

BENZEMA AFUNGUKA KUHUSU UTATA UNAOZINGIRA WIMBO WA FOTO MOTO

Msanii wa kundi la Ochungulo Family Benzema amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya Noti Flow kudai kuwa hajawahi faidi na mirabaha ya wimbo wao wa “Foto Moto.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Benzema amesema kipindi walimaliza kurekodi wimbo huo Noti Flow alimuambia kwamba ana haja na wimbo wa Foto Moto kwa kuwa muziki wa Kenya haulipi, jambo lilimfanya achukue wimbo huo na kuuweka kwenye mitandao ya kupakua na kusikiliza muziki.

Benzema amesema kwa sasa anaendelea kuingiza kipato kupitia mirabaha ya wimbo wa Foto Moto,  hivyo Noti Flow ndio wakulaumiwa kwa kuwa alikata tamaa mapema juu ya wimbo huo.

Utakumbuka wimbo wa Foto Moto wake Noti Flow akiwa amemshirikisha Benzema ilitoka mwaka wa 2020 na video yake kwenye mtandao wa youtube ina zaidi ya views millioni 4.5.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke