You are currently viewing Benzema afunguka kujiondoa Ochungulo Family

Benzema afunguka kujiondoa Ochungulo Family

Msanii Benzema amejibu tetesi za kujiondoa kwenye kundi la Ochungulo Family baada  ya kuonekana akifanya kazi zake binafsi.

Kwenye mahojiano na SPM Buzz Amesema yeye bado ni mwanafamilia wa Ochungulo ikizingatiwa kuwa kuna kazi nyingi ambayo wamefanya kwa pamoja kama kundi.

Aidha amekanusha kuwa kwenye ugomvi na wasanii wanaounda kundi hilo kwa kusema kuwa wana uhusiano mzuri wa ufanyaji kazi huku akiahidi mashabiki watarajie makubwa kwenye muziki wao mwaka 2023.

Utakumbuka Agosti 30 mwaka huu kundi la Ochungulo Family ambalo linaundwa na wasanii Nelly The Goon, Benzema na Dmore walitabariki na album iitwayo “Tamasha” ambayo ina jumla ya mikwaju 8 ya moto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke