You are currently viewing BEST NASO AACHIA RASMI EXTENDED PLAYLIST (EP) YAKE MPYA

BEST NASO AACHIA RASMI EXTENDED PLAYLIST (EP) YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva, Best Naso ameachia Extended Playlist (EP) mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

EP hiyo inakwenda kwa jina la Shujaa ina jumla ya nyimbo 11 za moto ikiwa na kolabo 8 kutoka kwa wakali kama Tunda Man, Dully Sykes, Nay wa Mitego, Stamina,Saida Karoli, Young Killer, Country Boy na Kala Jeremiah.

Shujaa ambayo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani  ina ngoma kama Number One,Beautiful, Kuoa, Bahati, Hero na nyingine nyingi.

Utakumbuka mwaka jana Best Naso aliachia albamu yake ya tatu, The Gift of Life yenye nyimbo 32.

Best Naso ameshaachia albamu kama Mamu wa Dar (2009) na Narudi Kijijini (2013), na zote zilifanya vizuri hasa ngoma zilizobeba majina ya albamu hizo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke