You are currently viewing BEST NASO MBIONI KUACHIA EP MPYA

BEST NASO MBIONI KUACHIA EP MPYA

Msanii wa Bongofleva Best Naso ameanika hadharani tracklist ya EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Sauti ya Hisia.

Kupitia Instagram yake Hitmaker huyo wa ngoma ya “Tamba” amesema EP hiyo ambayo ina jumla ya ngoma 11 ya moto itaingia sokoni rasmi Mei 15 mwaka 2022.

Best Naso amewashirikisha wakali kama Dully Sykes, Nay wa Mitego na Stamina huku EP yenyewe ikiwa na nyimbo kama Napendwa, Bahati, Tubadilike, Ajigambe, Single, Happy na nyingine nyingi.

Hii project ya kwanza kwa mtu mzima Best Naso kwa mwaka huu ikizingatiwa kuwa amekuwa akiachia ngoma mfululizo bila kupoa katika siku za hivi karibuni.

Utakumbuka mwaka wa 2021 mkali huyo wa muziki wa Bongofleva alitubariki na album iitwayo Gift of Life iliyokuwa na jumla ya mikwaju 32 ya moto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke