You are currently viewing BEYONCE ARIDHIA OMBI LA KUONDOA NENO “SP*Z”  KWENYE WIMBO WAKE “HEATED”

BEYONCE ARIDHIA OMBI LA KUONDOA NENO “SP*Z” KWENYE WIMBO WAKE “HEATED”

Hatimaye Beyonce amekubali kuondoa neno ambalo ni kero kwa walemavu kutoka katika wimbo wake uitwao “Heated” ulio kwenye album yake mpya iitwayo “Renaissance” wimbo ambao uliandikwa na rappa Drake na wengine.

Msemaji wa Beyoncé ambaye alitoa taarifa kwa vyombo vya habari, amesema kwamba neno hilo halikutumika makusudi ili kuwakejeli walemavu na litaondolewa.

Neno hilo ni “SP*Z” ufupisho wa “Spastic” ambalo maana yake ni mtu ambaye amepoteza uwezo wa kutumia vyema viungo vya mwili au hata akili na ni aina ya ugonjwa wa kupooza ubongo yaani Cerebral Palsy.

Utakumbuka, hili linajiri kwa Beyonce kufuatia mwezi mmoja kupita, mwanamuziki mwingine aitwae Lizzo nae kubadili neno hilo hilo ambapo alilitumia kwenye wimbo wake uitwao Grrrls.

Hannah Diviney, mmoja wa watetezi wa walemavu nchini Marekani, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba; kusikia matumizi ya neno hilo tena na Beyonce, ni kama kofi usoni mwake na kwenye nyuso za walemavu na hatua walizopiga na Lizzo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke