Mkongwe wa muziki wa Taarab nchini Tanzania Bi Khadija Kopa ambaye ni mama mzazi wa msanii kutoka WCB Zuchu Ameweka ujumbe ambao umewaacha watu wengi na maswali mengi katika mitandao yake ya kijamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Khadija Kopa amendika Ujumbe wa kumtakia kheri mwanae Zuchu katika maisha yake mapya ambayo yataanza siku ya Valentine Februari 14 ambapo amesema kila mwanamke ana ndoto ya kuishi maisha hayo.
“Zuhura mwanangu Nimekulea kwenye maadili na Najua wewe ni binti mwenye maamuzi sahihi na mimi kama Mama yako niseme sina budi kukusapoti .Tarehe 14 inaenda kua siku yako kubwa hakuna mwanamke asie na ndoto hii.M/Mungu akakusimamie najua hutoniangusha .siku hii isiwe tu siku yako kubwa duniani basi pia ikawe ndo mwanzo wa maisha mapya yenye Furaha .M/Mungu Akulinde kiziwanda changu Amin” ameandika Bi Khadija Kopa.
Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameibuka na kuhoji kuwa huenda siku hiyo zuchu akavishwa pete ya uchumba na bosi wake diamod platinumz ambaye katika siku za hivi karibuni amehusishwa kutoka kimapenzi na hitmaker huyo wa “Sukari.
Wengine wameenda mbali Zaidi na kusema kuwa huenda Zuchu akaachia album au E yake mpya siku hiyo ya wapendanao duniani ila ni jambo la kusibiriwa.