You are currently viewing BI KHADJA KOPA AMKINGIA KIFUA ZUCHU KWA UANDISHI WA NYIMBO

BI KHADJA KOPA AMKINGIA KIFUA ZUCHU KWA UANDISHI WA NYIMBO

Mama mzazi wa msanii Zuchu, Bi Khadja Omar Kopa amemkingia kifua binti yake huyo kutokana na kauli yake aliyotoa juzi kati kuwa asishindanishwe na wasanii wa kike kwenye uandishi wa nyimbo kwani itakuwa ni kuwaonea.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Bi Kopa amekiri kuwa Zuchu ni mwandishi mzuri wa nyimbo na haoni wa kushindana nae kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki.

Mkali huyo wa mipasho amewatolea uvivu wasanii wa kike wanaomkosoa Zuchu kwa kusema kwamba wengi wao wamekuwa wakibebwa na waandishi wa nyimbo kutokana na wao kuwa wazembe kwenye suala la uandishi.

Katika hatua nyingine amewajibu wanaodai kuwa Zuchu anabebewa na lebo ya WCB kwa kusema kuwa bidii yake ndio imempa mafanikio makubwa kwenye muziki, hivyo waache wivu kwani ndio imewarudisha nyuma kisanaa.

Hata hivyo amemalizia kwa kumjibu promota Ostaz Juma ambaye alidhalalisha Zuchu kimaumbile kwa kusema kwamba hana muda wa kugombana na jamaa huyo ambaye anatumia jina la mwanae kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke