You are currently viewing BIEN AFUNGUKA KUHUSU WASANII WA KIGENI KUTUMBUIZA KENYA

BIEN AFUNGUKA KUHUSU WASANII WA KIGENI KUTUMBUIZA KENYA

Msanii wa Sauti Sol Bien Aime Baraza amefunguka kuhusu suala la wasanii wa mataifa mengine kupewa kipau mbele kwenye hafla za kisiasa hapa nchini Kenya.

Akipiga stori na Mpasho, Bien amesema wasanii wa kigeni wanapotumbuiza nchini ni faida kwa wasanii wa ndani kwa kuwa wasanii wa Kenya pia hupokea upendo wanaposafiri nje ya nchi.

Mkali huyo wa ngoma ya “Inauma” ametaka wasanii wa kigeni kuruhusiwa kutumbuiza nchini bila kubaguliwa huku akiwataka wanaoshinikiza wasanii hao kupigwa marufuku kwenye majukwaa ya muziki nchini kuacha ubinafsi.

Katika hatua nyingine amempongeza aliyekuwa msanii wa Sol Generation Crystal Asige kwa kuteuliwa kama Seneta anayewakilisha watu wanaoishi na changamoto ya ulemavu nchini.

Bien amemtaja Crystal kama mwanamke mwenye akili sana huku akisema kwamba ana uhakika atawatumikia watu hao kwa uadilifu kwani ni jambo ambalo amekuwa akiliota kwa kipindi kirefu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke