Msanii wa Sauti Sol Bien amekanusha kuwa kwenye ndoa ya wazi na mke wake Chiki Kuruka baada ya kauli yake hiyo kuleta ukakasi miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii.
Akipiga stori na Mungai Evei Bien amesema yeye hamiliki mke wake kama namna ambavyo wanaume wengi wa kiafrika wanavyofanya wanapokuwa kwenye ndoa bali waliamua kuja pamoja kwa ajili ya kufanikisha ndoto zao kama wanandoa.
Hitmaker huyo wa “Mbwe Mbwe” amefunguka kuwa swala la kucheat sio swala la kufanya kuachana na Mwenza wako.
Lakini pia ameshauri kuwa sio kitu kizuri kwa wanandoa kubadilishana neno la siri la Simu.
“Kuna vitu vingi ambavyo unajenga na mke wako ambavyo ni zaidi hisia za wivu katika mahusiano yako. Sidhani kucheat ni msingi wa kuachana na mtu. Kuna mambo mabaya zaidi ambayo mtu anaweza kukufanyia,” amesema Bien Aime sol .