You are currently viewing BIEN ATOA YA MOYONI KUHUSU ERIC OMONDI KULETA MAGEUZI KWENYE MUZIKI KENYA

BIEN ATOA YA MOYONI KUHUSU ERIC OMONDI KULETA MAGEUZI KWENYE MUZIKI KENYA

Msanii wa Sauti Sol, Bien amedai kwamba anaunga mkono harakati za  mchekeshaji Eric Omondi kuleta mabadiliko kwenye tasnia ya muziki nchini.

Katika mahojiano na Plug tv, Bien amesema kitu ambacho kinamfanya wakati mwingine kutofautiana kimawazo na Eric Omondi ni kutokana na mchekeshaji huyo kuingiza kiki nyingi kwenye masuala muhimu.

Bien amesema licha ya kwamba wamekuwa wakitupia maneno makali mtandaoni na Eric Omondi, anaheshimu kila ambacho mchekeshaji huyo anakifanya kwa kuwa anajituma sana kwenye shughuli zinazomuingizia kipato.

Katika hatua nyingine Bien amewataka wakenya waache kasumba ya kuwashambulia watengeneza maudhui na badala yake wawe mstari wa mbele kuunga mkono shughuli zao kwani kuwakosa kila mara ni ulimbukeni wa hali ya juu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke