Mwimbaji mkuu wa Kundi la Sauti Sol nchini Kenya Bien amesema hashauri watu waliopo katika umri wa miaka ya ishirini kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwani ni kupotezeana muda.
Bien amesema watu walio katika umri huo wanapaswa kujijali wenyewe na kusafiri kwa kuwa mtu aliyeko katika umri huo bado anajitafuta ajue kitu gani hasa anakihitaji. “Siwezi kumpa ushauri mtu mwenye umri wa miaka ishirini awe kwenye mahusiano, ni kupoteza muda, angalau fanya kazi, usafiri pia uwe na watu wengine huku na huko.” alisema Bien.
Aidha aliongeza kwamba mtu akiwa katika umri huo hajitambui na mtu aliye naye pia hajitambui “Unadhani unafanya nini? Mnajaribu kusuluhisha mambo pamoja lakini mwisho wa siku yaani nadhani ni bora kuwa peke yako ikiwa uko katika miaka ya 20” alimaliza Mwanamuziki huyo.