You are currently viewing BIEN: SILALI CHUMBA KIMOJA NA MKE WANGU

BIEN: SILALI CHUMBA KIMOJA NA MKE WANGU

Msanii wa kundi la Sauti Sol Bien kwa mara nyingine tena ameibuka na kauli yenye utata kuhusu maisha yake na mkewe Mtangazaji Chikki.

Akipiga stori na Mambo Mseto ya Radio Citizen Bien amesema licha ya mkewe kuwa Meneja wake, wanaposafiri kwa ajili ya show kila mmoja hulala chumba chake.

“Katika ndoa yetu kuna mipaka pia, kwa mfano kama nimeitwa mahali niko na shoo, nakaa kwa chumba cha hoteli mimi peke yangu. Huwa sitaki hata muziki hapo ndani. Nataka tu kukaa peke yangu nijisikilize na kujitathmini kuhusu jinsi nitakavyoifanya hiyo shoo” alisema.

“Kwa hiyo kama unaniita kama ajenti ama promota, huwezi nitengea chumba kimoja mimi na mke wangu, sitaki kulala na yeye kitanda kimoja hiyo siku, nataka kuenda kujisikilizia,” alisema Bien.

Hittmaker huyo wa ngoma ya “Inauma” amefafanua kwamba wakienda kwa shoo na mke wake mambo ya uchumba yanabaki nyumbani na kule wanaenda kama msanii na Meneja wake na kwa hiyo kuna umuhimu wa kila mmoja kutengewa chumba chake binafsi mbali na mwingine.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke