You are currently viewing BIEN SOL NA AARON RIMBUI KUIDONDOSHA EP YAO MPYA, IJUMAA HII

BIEN SOL NA AARON RIMBUI KUIDONDOSHA EP YAO MPYA, IJUMAA HII

Kama wewe ni shabiki wa Msanii wa Sauti Sol Bien na Aaron Rimbui kaa tayari kwa ajili ya EP ya pamoja kutoka kwa wakali hao.

Kupitia kurasa zao za instagram Bien na Aron wameachia Cover rasmi ya EP yao mpya iitwayo “Bald men Love Better” ambapo wamesema uzinduzi wa EP hiyo utafanyika Novemba 6 mwaka huu jijini Nairobi.

Wameenda mbali zaidi na kusema kwamba EP hiyo inatarajiwa kuachiwa rasmi Novemba 5 mwaka huu na mashabiki wanaweza kui-pre-order kupitia majukwaa ya muziki kama Spotify na Apple music.

Tayari Bien na Aaron Rimbui wameachia wimbo uitwao Bald men Anthem, moja kati ya singo inayopatikana kwenye Bald Men Love Better EP.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke