You are currently viewing BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU KUPANGA UZAZI

BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU KUPANGA UZAZI

Msanii kutoka kundi la Sauti Sol Bein Aim Baraza amesema kuwa yupo tayari kukata mshipa wa uzazi maarufu vascectomy punde atakapo pata watoto na mke wake Chiki Kuruka.

Akizungumza kwenye kipindi cha Baldmen Session kwenye mtandao wa youtube Bein amesema kuwa kupanga uzazi barani Afrika ni swala ambalo limewachiwa wanawake.

Bien amesema kuwa hawezi kumwachia mke wake mzigo huo pekee licha ya kuwa wanaume wengi wanaogopa kufanyiwa vasectomy.

“Wanaume wengi hawako tayari kufanyiwa vasektomi lakini mimi niko tayari kuangalia vasektomi, nimechoka kuweka mzigo huu kwa vifaranga wetu, kwanza najua dawa mbalimbali za uzazi wa mpango zina madhara tofauti. “Amesema Bien kwenye kipindi anachoandaa.

Lakini pia amefunguka kuwa mashabiki wamekuwa wakimshinikiza kupata mtoto na mke wake Chiki Kuruka licha ya kuwa kwenye ndoa kwa miezi 18 pekee.

“Hata mimi Wakenya wameniangalia weird, I’ve stayed karibu for 18 months na sijafanya kitu lakini kila kitu na time yake,” alisema.

“Sijawahi kuwa na hamu ya kuzaliana! Kwa hiyo haijawahi kunisumbua sana.” amesema

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke