Mwana kikundi wa Sauti Sol, Bien amefunguka namna uchaguzi nchini Kenya ulivyoendeshwa.
Katika mahojiano na Mungai Eve, Bien amesema mchakato mzima wa uchaguzi mkuu nchini ulikuwa wa haki na huru ambapo amewapongeza wakenya kwa kudumisha Amani kabla na hata baada ya uchaguzi.
Hitmaker huyo “Inauma” amewataka wakenya kurejea kazini baada ya Rais mteule William Ruto kutangazwa na Tume huru ya uchaguzi IEBC hata kama kuna wale ambao hawakuridhishwa na matokeoa ya urais.
Bien ametoa wito kwa serikali mpya itakayoingia mamlakani kuboresha sanaa nchini Kenya ili vijana waweze kupata ajira.
Kuhusu mgogoro wao na muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja kutumia wimbo wao wa “Extravangaza bila ridhaa ya Sauti Sol, Bien amesema mawakili wao wanashughulikia suala hilo kuhakikisha wanapata haki.