You are currently viewing Bien wa Sauti Sol ajibu madai ya Crystal Asige kufungua kesi mahakamani dhidi ya Sol Generation

Bien wa Sauti Sol ajibu madai ya Crystal Asige kufungua kesi mahakamani dhidi ya Sol Generation

Mwimbaji wa Sauti Sol amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya aliyekuwa msanii wa Sol Generation Crystal Asige kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya bendi hiyo maarufu kwa kukiuka mkataba wake.

Akizungumza na Mpasho, Bien amesema bendi ya Sauti Sol iko tayari kukutana na seneta huyo mteule ambaye anawakilisha watu wanaoishi na ulemavu, mahakamani kupata mwanga kuhusu mgogoro unaozingira mkataba wake na lebo ya Sol Generation.

“Tukutane kortini na kuweka hati zetu zote mezani. Tunaweza tu kufuata njia aliyochagua. Masuala hayo yanaweza kushughulikiwa vyema mahakamani kama alivyofanya,” Bien alisema.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Asige anaitaka mahakama kuwashurutisha wasanii wa Sauti Sol kuweka wazi kiasi cha pesa ambacho walipata kutoka kwa nyimbo alizoshirikisha tangu mwaka 2019.

Nyimbo hizo ni pamoja na Lenga, Extravaganza, Ukiwa Mbali, Intro na Favourite Song.

Lakini pia anaitaka mahakama kuagiza kundi la Sauti Sol kumlipa fidia huku akisisitiza wawasilishe taarifa zote za leseni kuhusu nyimbo alizoshirikishwa.

Crystal Asige ameishtaki Sol Generation Records Limited, Bien-Aime Baraza, Polycarp Otieno, Willis Chimano, Delvin Mudigi na KLM Royal Dutch Airlines Kenya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke