You are currently viewing BIEN WA SAUTI SOL AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA MUUNGANO WA KISIASA WA AZIMIO LA UMOJA

BIEN WA SAUTI SOL AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA MUUNGANO WA KISIASA WA AZIMIO LA UMOJA

Msanii wa Sauti Sol, Bien amefunguka na kudai kuwa hana ugomvi wowote na muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja kama namna baadhi ya watu wanavyochukulia mtandaoni.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Bien amesema kile ambacho anakishinikiza kama kundi la Sauti Sol  malipo yao wimbo wa Extravangaza ambao ulitumiwa na muungano huo kwenye shughuli zao kisiasa bila ridhaa yao.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mbwe Mbwe” amesema mawakili wapo kwenye mazungumzo na Uongozi wa Azimio la Umoja kutatua utata unaozingira wimbo wao  wa extra vangaza huku akidokeza kwamba huenda wakalipa shillingi billioni moja za kenya kwa kuharibiwa brand yao ya muziki.

Kauli ya Bien imekuja mara baada ya Ezekiel Mutua kuitaka bendi ya Sauti Sol kuacha kushiriki vita vya mtandaoni na muungano wa Azimio la Umoja na badala yake watumie njia ya mazungumzo kutatua tofauti zao kudai haki yao kwani jambo hilo huenda likaathiri muziki wao.

Utakumbuka baada ya Sauti Sol kutishia kuufungulia muungano wa Azimio la Umoja kesi kwa kuitumia wimbo wa Extravaganza kwenye kampeini zao bila ridhaa yao, walipoteza takriban subscribers 2,000 kwenye mtandao wa Youtube na kuifanya channel yao kushuka kutoka subscribers elfu 905 hadi 904.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke