Mwanakikundi wa bendi ya Sauti Sol, Bien Barasa ameendelea kutoa ushuhuda wa ndani kuhusu maisha yake, amefunguka kwamba aliwahi kutaka kuivunja ndoa yake.
Kwenye podcast ya Bald Box msanii huyo amesema kwamba mwaka wake wa kwanza kwenye ndoa nusra ampe talaka mke wake Chiki kuruka baada ya kupitia wakati mgumu kipindi cha korona.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “MbweMbwe” amesema alipatwa na msongo wa mawazo kipindi cha korona baada ya shughuli za kimuziki za bendi ya Sauti Sol kusambaratika lakini alikuja akapata afueni alipopata ushauri nasaha kutoka kwa mwanasaikolojia.
Utakumbuka Bien Aime Barasa na mkewe Chiki Kuruka ambaye ni dancer, mwalimu wa mazoezi ya mwili na mtangazaji wa redio walifunga ndoa miaka miwili iliyopita.