You are currently viewing HARMONIZE NA ERIC OMONDI WAMALIZA TOFAUTI ZAO

HARMONIZE NA ERIC OMONDI WAMALIZA TOFAUTI ZAO

Wasanii Harmonize  na Eric Omondi hatimaye wamemaliza tofauti zao kwa kusameheana kufuatia matukio yaliyojiri Jumapili Mei mosi, 2022.

Baada ya uvumi wa ugomvi wake na Harmonize, Eric Omondi ameomba radhi kutokana na kisa hicho ambacho kinadaiwa kuwafanya yeye na nyota huyo kutoka Tanzania kukaa karibu siku nzima katika kituo cha polisi cha Kileleshwa jijini nairobi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Eric Omondi ameweka wazi kuwa walisuluhisha changamoto iliyopelekea kukosekana kwa maelewano kati yao.

“Kama kaka mkubwa, kama mshereheshaji na kama msanii mwenzangu wa Afrika Mashariki nataka kuomba radhi kwa yote yaliyotokea,” Eric alisema.

Kwa upande wa Harmonize alisema hakuna aliyekamilika na kuongeza kuwa anachukulia kilichotokea kama sehemu ya changamoto za kazi na si vinginevyo huku akikanusha kumshambulia Eric Omondi kwa ngumi.

“Bado mimi na kaka yangu tunampenda na kumheshimu hakuna mtu mkamilifu katika dunia hii, mimi niko poa kutoka moyoni mwangu. Kilichotokea ni changamoto za kazi tu na katika ulimwengu huu huwezi kuwa na furaha siku zote sisi ni ndugu,” Harmonize amesema katika instastory yake Instagram.

Ikumbukwe Harmonize alikamatwa wikiendi hii iliyopita na kushikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kileleshwa kwa madai ya kukiuka makubaliano ya kutokea kwenye club kadhaa za jijini Nairobi baada ya malipo kutolewa. Inasemekana Eric Omondi ndiye alipokea malipo hayo kwa niaba ya Harmonize.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke