Msanii anayeunda kundi la Sauti Sol, Bien Baraza amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kusema kwamba hatawahi kuwa na amani hadi pale bei ya unga itakaposhuka.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Bien amedai kwamba moja kati ya bidhaa ambayo anatamani ishuke bei ni unga wa sima huku akipendekeza iuzwe shillingi 99 za Kenya
“You won’t see me smiling till the price of unga goes down to Ksh. 99 #Inauma”, Aliandika
Hata hivyo wafuasi wake wameonekana kumfanyia mzaha kwenye uwanja wa comment ya posti yake kwa kusema kwamba itabidi azoee huku wengine wakihoji kuwa anashinikiza bei ya unga wa sima ishuke kwa kuwa anatokea katika jamii ya Waluhya ambayo imekuwa ikihusishwa sana na uraibu wa ugali.