You are currently viewing BIEN WA SAUTI SOL ATANGAZA KUWEKEZA ZAIDI KWENYE ISHU YA KUFANYA KOLABO NA WASANII WENGINE KAMA MSANII UHURU

BIEN WA SAUTI SOL ATANGAZA KUWEKEZA ZAIDI KWENYE ISHU YA KUFANYA KOLABO NA WASANII WENGINE KAMA MSANII UHURU

Msanii wa Sauti Sol, Bien amefunguka na kudai kwamba mwaka huu atajikita zaidi kwenye suala la kufanya kolabo na kuwashirikisha wasanii wengine kwenye kazi zake atakazo achia.

Katika mahojiano na mpasho Bien amesema kuwa amepokea maombi nyingi za wasanii wanaotaka kufanya naye kazi huku akidokeza ujio wa album mpya ya kundi la Sauti Sol ambayo itaingia sokoni mwezi Aprili mwaka wa 2022.

Kauli ya Bien inakuja wakati kundi la Sauti Sol linajianda kufanya ziara yao ya kimuziki  Barani Ulaya kuanzia Aprili Mosi, mwaka huu huko Barcelona nchini Uhispania na itafanyika ndani ya miji 19 kwa kipindi cha mwezi mmoja..

Ziara hiyo inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Ujerumani, Ureno, Ufaransa, Denmark, Uingereza, Belgium ambapo kilele chake kitakuwa nchini Uholanzi Juni 28 mwaka wa 2022.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke