You are currently viewing BIEN WA SAUTI SOL ATOA OFA  KWA YEYOTE ATAKAYEMREJESHEA SIMU YAKE ILIYOIBIWA

BIEN WA SAUTI SOL ATOA OFA KWA YEYOTE ATAKAYEMREJESHEA SIMU YAKE ILIYOIBIWA

Member wa Sauti Sol, Bien ameahidi kutoa ofa ya shillingi elfu 50 kama zawadi kwa yeyote atakayemrudishia simu yake ambayo juzi kati iliibiwa katika ukumbi wa burudani wa Carnivore kwenye onesho la NRG Wave Concert.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Bien ameandika ujumbe wa masikitiko kwa kusema kwamba aliibiwa simu aina ya Infinix Note 11 Pro na vifunguo vya gari aina ya Porsche Cayenne ambapo amedai kuwa simu yake ilikuwa na data muhimu ya album mpya ya Sauti Sol ambayo inatarajiwa kuingia sokkoni mwezi Aprili mwaka huu.

Hitmaker huyo wa “Mbwe Mbwe” ameenda mbali zaidi na  kutania kuwa hangekaa vibaya watu wangemuibia hata mke wake Chiki Kuruka huku akisisitiza kutoa zawadi ya shillingi elfu 50 kwa yeyote atakayemrudhishia simu pamoja na vifunguo vya gari.

Sanjari na hilo msanii Ndovu Kuu amethibitisha kuibiwa simu kwenye onesho la NRG Wave Concert lilofanyika katika ukumbi wa Carnivore ambapo pia ameahidi kutoa zawadi kwa yeyote atakayemregeshea simu yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke