You are currently viewing BIEN WA SAUTI SOL AUCHANA MUUNGANO WA KISIASA NCHINI KENYA AZIMIO LA UMOJA

BIEN WA SAUTI SOL AUCHANA MUUNGANO WA KISIASA NCHINI KENYA AZIMIO LA UMOJA

Mwanakikundi wa Sauti Sol, Bien ameamua kurusha jiwe gizani kwenda kwa uongozi wa Azimio la Umoja unaongozwa na Raila Odinga baada ya bendi hiyo kupoteza jumla ya subscribers 2.000 kwenye mtandao wa youtube ndani ya kipindi cha masaa 48.

Kupitia Mtandao wa Instagram Bien, ameandika ujumbe wa kimafumbo ambao umetafsiriwa na wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii kuwa bendi hiyo inaegemea upande wa mrengo wa Kenya Kwanza unaongozwa na Naibu wa Rais Dakta William Ruto wakati huu taifa inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

“Time will reveal. Wale wanashuka washuke saa hii. Stage yao imefika.” Ameandika Instagram.

Chapisho hilo kutoka kwa Bien imeibua hisia mbali mbali miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii, ambapo wengi wamewataka wasaani hao bendi hiyo kujitenga na masuala ya siasa na badala yake wawekeze nguvu zao kwenye suala la kutoa muziki mzuri.

Channel ya Youtube ya Sauti Sol ambayo ilikuwa na subscribers elfu 903 kwa sasa ina jumla ya subscribers elfu 903.

Jumatatu wiki hii bendi ya Sauti Sol ilitishia kuushtaki Muungano wa Azimio la Umoja kwa kutumia wimbo wao “Extravaganza” bila ridhaa yao kwenye kampeni zao ambapo siku hiyo walikuwa wakimtambulisha Mgombea mwenza wa Raila Odinga, Bi. Martha Karua.

Utakumbuka mwaka wa 2021 Sauti Sol walikuwa baadhi ya wasanii Kenya waliojitokeza hadharani na kupinga mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho kupitia Mpango wa Maridhiano BBI ambao ulikuwa unaongozwa na kinara wa ODM Raila Odinga.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke