Mwiimbaji wa Sauti Sol Bien Aime Baraza amefunguka na kudai kuwa atawafunza watoto wake lugha ya kiluhya ambayo ndio chimbuko lake.
Katika mahojiano na mpasho Msanii huyo amewahimiza wazazi kuwafunza watoto wao lugha yao ya mama kama njia moja ya kudumisha utamaduni, mila na desturi za kiafrika.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Mbwe mbwe ameeleza kuwa ana mpango wa kuachia kitabu chake cha hadhithi kiitwacho Bald Man Comic ambacho ni mahusisi kwa ajili ya kusherekea na kutambua mchango wa utamaduni wa kiafrika kupitia fasihi andishi.
Huu ni muendelezo mzuri kwa wasanii wa sauti sol ambao katika siku za hivi karibuni wamegeuza muziki wao kuwa biashara ambapo wamewekeza kwenye nyanja mbali mbali kama njia ya kujiongezea kipato.