Mwanamuziki wa Sauti Sol, Bien ametoa changamoto kwa wasanii nchini kuanza kutumia lugha ya kiingereza kwenye nyimbo zao ili muziki wa Kenya uweze kufika mbali zaidi.
Bien amesema licha ya wasanii wa Kenya kutoa muziki mzuri wengi wao wamekuwa wakitumia lugha ya Sheng kwenye nyimbo zao jambo analosema limewafanya wasanii kushindwa kutanua wigo wa muziki wao kimataifa.
Katika hatua nyingine Bien amekiri kuwa hakuwa anajitambua kimuziki kabla ya wasanii wa kundi la Sauti Sol kuanza kufanya kazi zao kama wanamuziki wa kujitegemea.
Hitmaker wa “Inauma” amesema amejifunza mambo mengi kama msanii huru ikiwemo kutayarisha na kuandilka nyimbo zake mwenyewe.