Msanii wa Sauti Sol bien amemtolea uvivu Mwenyekiti wa Chama cha Hakimiliki na Muziki nchini Ezekiel Mutua baada ya kudai kuwa alipewa mamlaka ya kutoa kibali kwa nyimbo zao kutumika kwenye shughuli za kibiashara.
Katika mahojiano na Eve Mungai, Bien amesema ameshangazwa na hatua ya Mutua kutoa ruhusa ya wimbo wa “Extrangaza” kutumika kwenye shughuli za muungano wa Azimio la Umoja bila idhini yao ikizingatiwa kuwa walitumia kiasi cha shillingi millioni 2 za Kenya kutayarisha video ya wimbo huo.
Aidha ameenda mbali zaidi na kusema kuwa Ezekiel Mutua hajui majukumu yake kwani alipewa wadhfa huo kuangazia maslahi ya wanasiasa.
Hata hivyo amedokeza kuwa wanaendelea na mazungumzo na uongozi wa azimio la umoja kupata suluhu ya mgogoro uliobuka kati yao huku akitoa wito kwa mashabiki waendelea kusikiliza na kucheza nyimbo zao kwenye maeneo ya umma.