You are currently viewing BIFU LA KRG THE DON NA KUNDI LA MBOGI GENJE LACHUKUA SURA MPYA

BIFU LA KRG THE DON NA KUNDI LA MBOGI GENJE LACHUKUA SURA MPYA

Inaonekana bifu ya Mbogi Genje na Krg The Don haitapoa hivi karibuni hii ni baada ya wasanii wa kundi hilo kuibuka na kumchana Krg The Don kutokana na kauli aliyotoa majuzi kuwa wasanii wa mbogi genje ni wasanii wa mashinani.

Wakiwa kwenye moja ya Interview wasanii hao wakiongozwa na Militant wamesema Krg The Don aache kujipiga kifua kuwa ni msanii wa kimataifa wakati ana idadi ndogo ya wafuasi kwenye mitandao kustream muziki duniani huku wakisema kama kweli Krg The Don angekuwa na pesa angewalipa baada ya kufanya nao kolabo kupitia wimbo wa Zible.

Wasanii hao wa Mbogi Genje wameenda mbali zaidi na kusema kuwa hawana muda wa kupishana na Krg The Don ila hawakufurahishwa na hatua ya msanii huyo kukiuka mkataba wa maelewano kuhusu umiliki wa wimbo wa Zible baada ya kupakia video ya wimbo huo kwenye Youtube channel yake bila ridhaa yao.

Mapema wiki Krg The Don aliibuka na kuwachana wasanii Mbogi Genje kuwa hawakugharamia chochote kwenye mchakato wa kuandaa audio na video wa wimbo wa Zible,  hivyo hawana haki ya kudai umiliki wa wimbo huo.

Hii ni baada ya mbogi genje kudai kuwa Krg The Don aliwasiliti baada ya kukiuka mkataba wa maelewano kuhusu umiliki wa wimbo wa Zible alipoahamua kupakia video wa wimbo huo kwenye channel yake ya youtube bila idhini yao

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke