You are currently viewing BIFU LA RAPA LIL DURK NA NBA YOUNGBOY LACHUKUA SURA MPYA

BIFU LA RAPA LIL DURK NA NBA YOUNGBOY LACHUKUA SURA MPYA

Rapa kutoka nchini Marekani Lil Durk amevunja kimya chake kuhusu kinachoendelea mtandaoni kati yake na NBA Youngboy.

Lil Durk kupitia ukurasa wake wa instagram amepost picha akiwa amelalia pesa nyingi na kuandika ujumbe “mpuuzi” uliotafsiriwa kuwa ni jibu kwa NBA Youngboy

Lil Durk ametoa kauli hiyo baada ya rapa NBA Youngboy kum-diss pamoja na label ya O’block kwenye ngoma yake mpya Bring The Hook & Know Like I Know ambapo amewatolea kauli chafu lakini pia kumtishia lil durk kwamba atakufa “young n**ga gone die…stay safe”

Lakini pia kupitia ngoma hiyo amem-diss rapa nlechoppa kwa kuingilia bifu kati yake na watu wa (o’block) label inayomilikiwa na lildurk, akidai kwamba anaingilia bifu lisilomhusu

NBA Youngboy kupitia ngoma hiyo amesikika kwenye mstari akisema (you could say i was you favourite n**ga better stay up in your place b****h) yaani ulisema kwamba ulikuwa unanikubali lakini ni bora ukabaki katika nafasi yako mpuuzi wewe.

Utakumbuka NBA Young aliachia disstrack hiyo kufuatia NLE Choppa kumtwanga ngumi shabiki yake baada ya kuingia kwenye ugomvi  wakiwa uwanja wa ndege.

Sababu ya ugomvi huo inasemekana kuwa ni baada ya NLE Choppa kufanya moja ya interview hivi karibuni na kusema kwamba hapo awali NBA Young boy alikuwa moja kati ya wasanii wake anaowakubali zaidi lakini kutokana na ngoma yake mpya “Bring the Hook” aliyowa-diss  genge la O’block na marehemu King Von ameamua kumkataa

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke