Inaonekana ugomvi wa msanii Ringtone na DJ Mo hautapoa hivi karibuni, hii ni baada msanii huyo kuibuka na kumzushia DJ Mo kashfa zito.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Ringtone amemtuhumu DJ Mo kuwa yeye ndiye chanzo cha muziki wa injili nchini Kenya kusuasua katika siku za hivi karibuni.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sisi Ndio Tuko” amesema DJ Mo aliua vipaji vingi kwenye muziki wa injili kwa kuhitisha rushwa ya ngono kutoka kwa wasanii wa kike ili acheze nyimbo zao alipokuwa anafanya kazi kwenye runinga moja hapa nchini.
Hata hivyo DJ Mo hajajibu chochote kuhusiana na tuhuma hizo ila ni jambo la kusubiriwa.
Utakumbuka ugomvi wa Ringtone na DJ MO ulianza wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa album ya msanii Size 8 na hiii ni baada ya Ringtone kukatazwa kujiunga na makasisi waliokuwa wapewa nafasi ya kuibariki album ya Size 8, “Christ Revealed”.