You are currently viewing BIFU LA WEEZDOM NA MANZI WA TRM LACHUKUA SURA MPYA, WARUSHIANA MATUSI MTANDAONI

BIFU LA WEEZDOM NA MANZI WA TRM LACHUKUA SURA MPYA, WARUSHIANA MATUSI MTANDAONI

Msanii wa muziki Weezdom ameingia tena kwenye Headline kwenye mitandao ya kijamii kwa kumkingia kifua mpenzi wake Mylee Stacy baada ya mrembo aitwaye Manzi wa TRM kumchafua mtandaoni na kashfa za uongo.

Kupitia kwenye mtandao wa Instagram Weezdom ameonekana kukasirishwa na kitendo cha Ex wake huyo kumchafua Mylee Stacy na stori za kutunga ambapo amemporomoshea matusi mazito Manzi wa TRM akimtaka akome kumzungumzia vibaya Mylee Stacy mtandaoni.

Msanii huyo  amemtaka manzi trm akubali kwamba mahusiano yao yalivunjika kitambo badala ya kumkosesha Mylee Stacy Amani kwa kutumia jina lake kujitafutia umaarufu mtandaoni.

Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kutofurahisha na kitendo cha Weezdom kumtolea mambo mazito ex wake Manzi wa TRM ambapo wamemshauri wangetatua tofauti zao nje ya mitandao ya kijamii kwani wanajiahibisha wenyewe.

Utakumbuka hatua ya weezdom kumshushia matusi Manzi wa TRM imekuja siku chache baada ya kumuomba msamaha mpenzi wake Mylee Stacy kwa kitendo cha kumporeshea matusi mazito mtandaoni ambapo alienda mbali zaidi na kuahapa kutorudia kitendo cha kuwavunjia wanawake heshima.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke