You are currently viewing BIG SEAN AFUNGUKA KUWA ANAMDAI KANYE WEST TAKRIBANI SHILLINGI MILLIONI 670

BIG SEAN AFUNGUKA KUWA ANAMDAI KANYE WEST TAKRIBANI SHILLINGI MILLIONI 670

Sekeseke la Kanye West na Big Sean linazidi kupamba moto, hii ni baada ya YE kusema kwamba kumsaini Big Sean kwenye label yake, GOOD MUSIC mwaka wa 2007 ilikuwa ni kitu kibaya zaidi ambacho amewahi kukifanya kwenye maisha yake.

Sasa baada ya Kanye West kutoa kauli hiyo kwenye mahojiano na Drink Champs kupitia Revolt TV, Big Sean amekuwa akiangusha tweet mbali mbali akidai kwenda kwenye Podcast hiyo kujibu mashambulizi.

Lakini tweet iliyoibua uzito zaidi kwenye mtandao wa Twitter ni ile ambayo alisema anamdai Kanye West takribani  shilling million 670 za Kenya.

Tweet hiyo tayari ameifuta, hivi karibuni Sean alitangaza kuanzisha label yake na kuachana na GOOD Music ambayo alidumu nayo kwa miaka 14

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke