Rapa kutoka nchini marekani Big Sean amesema anampenda sana Kanye West na anampa heshima zote kwa upendo aliomuonesha kumshika mkono hadi kufahamika, lakini kwa alichokisema kwenye mahojiano na Drink Champs mwezi Novemba mwaka huu ni ujinga mtupu.
Big Sean amekuwa mgeni mpya wa Drink Champs, kipindi ambacho kitaruka Jumamosi hii, Sean amesikika akisema “Nampenda Kanye. Nampenda kwa nafasi aliyonipatia na kila kitu. Lakini nafikiri alichokisema kilikuwa ni upuuzi na ujinga mtupu.” amesema Big Sean.
Kanye West aliingia kwenye headlines baada ya kusema kwamba miongoni mwa vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ni kumsaini rapa Big Sean kwenye label yake, GOOD Music.