You are currently viewing BILLIE EILISH AJUTA KUTIZAMA VIDEO ZA NGONO AKIWA MDOGO

BILLIE EILISH AJUTA KUTIZAMA VIDEO ZA NGONO AKIWA MDOGO

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Billie Eilish amesema kutazama video za ngono mtandaoni kuliharibu ubongo wake kwani alianza kuzitazama akiwa mdogo.

Billie ambaye kwa sasa ana miaka 19 amesema hay wakati akihojiwa kwenye The Howard Stern Show.

“Kama mwanamke, nadhani video za ngono ni aibu,” alisema kwenye mahojiano hayo. “Nilikuwa naziangalia sana, kusema ukweli. Nilianza kuangalia pindi nina miaka 11.”

Aliendelea,” Nadhani ziliharibu kabisa ubongo wangu na najihisi kuvunjika kabisa kuwa niliangalia sana.”

Hitmaker huyo “Lovely” amekiri kuwa ilifika wakati alikuwa akiangalia video zenye vitendo vya kutisha na kikatili zaidi.

“Nilikuwa bikira. Nilikuwa sijafanya chochote. Na pia ilinipelekea kwenye matatizo.Mara ya kwanza nafanya mapenzi nilikuwa sikatai vitu ambavyo havikuwa vizuri. Kwasababu nilidhani hivyo ndivyo nilipaswa kuvutiwa navyo,” alisisitiza. “Nina hasira sana kuwa video hizo zinapendwa. Na nina hasira kwangu mwenyewe kwa kudhani ilikuwa sawa.”

Muimbaji huyo amekiri kuwa zilimfanya kuwa na fikira zenye kasoro kuhusu tendo la ndoa na mahusiano.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke